Ruka hadi Yaliyomo

Tume (ambayo sasa haipo) ya Utekelezaji wa Katiba (CIC) na Shirika la Kimataifa la Bajeti (IBP) walichapisha toleo lenye kichwa “Mambo 50 Mkenya Anapaswa Kujua Kuhusu Usimamizi wa Fedha za Umma Kuambatana na Katiba”.

Toleo hili linajibu masuala mbalimbali ambayo yamekuwa yakiulizwa na wananchi kuhusiana na masuala ya fedha za umma katika Katiba na Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma.

Sheria ya kusimami fedha za umma iliundwa ili kuwezesha kuetekeleza Sura ya 12 ya Katiba kuhusu usimamizi wa fedha za umma.

Toleo hili linakusudia kutoa uelewa wa vipengele muhimu vya Katiba na Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma ili kuwezesha ushiriki wa wananchi katika mchakato wa fedha za umma, ambao ni mojawapo ya maadili ya kitaifa na hitaji la Katiba.

Toleo hili limeandaliwa katika msururu wa maswali ambayo mtu wa kawaida anaweza kuuliza kuhusu mchakato wa bajeti ya Kenya na masuala mengine ya kifedha. Maswali haya ni kama ifuatavyo–

1. Majukumu ya jumla ya raia katika matayarisho ya bajeti

  1. Sheria ya kusimamia fedha za umma zinahusu nini na kwa nini nijali kuzifahamu?
  2. Majukumu yangu ni yapi kuhusu jinsi serikali inavyotumia fedha za umma?
  3. Je, kuna sheria inayoniwezesha mimi kama raia kushiriki katika harakati za bajeti?
  4. Je, Naweza kushiriki tu kama mtu binafsi au naweza kushirikiana na makundi ya watu
  5. Kwa hiyo kuna haki ya kushiriki katika Katiba, lakini vipi kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma?

2. Ratiba ya maandalizi ya bajeti ya kitaifa

  1. Nijitayarishe kushiriki katika maandalizi ya bajeti wakati gani?
  2. Tunaweza kuisoma taarifa kuhusu sera za bajeti inapotangazwa, lakini nitashiriki kivipi kutoa maoni yangu wakati inapotayarishwa?
  3. Ni wakati gani tunaweza kuona mapendekezo ya serikali kuhusu bajeti (Pamoja na maelezo ya makadirio) na kiwango cha fedha kilichotengewa sekta ya Elimu na afya?
  4. Je, idara ya mahakama hutengeneza bajeti yao na kuituma bungeni?
  5. Labda sikuelewa, lakini mapendekezo ya serikali kuhusu bajeti hutangazwa kwa umma wakati gani? Inasemekana kwamba lazima itumwe bungeni mwezi Aprili 30, lakini raia wataiona lini?

3. Majukumu ya bunge katika matayarisho ya bajeti ya kitaifa

  1. Kuna kiwango cha idadi ya mabadiliko tunayoweza kuomba bunge kutekelaza katika mapendekezo ya bajeti?
  2. Je, kila mwaka kati ya mwezi Aprili 30 na Juni 30, bunge linaweza kufanyia mabadiliko mapendekezo ya bajeti, mradi tu wasisababishe upungufu wa fedha, na raia wanaweza kushiriki katika mjadala pamoja na wabunge wakati wowote katika muda uliotengwa? Kwa hivyo kuna muda wa kutosha wa miezi 2 siyo?
  3. Je, kamati ya bunge kuhusu fedha na bajeti hupokea vipi maoni ya umma?
  4. Nafahamu kwamba tangu kitambo, bajeti huidhinishwa kabla mwaka wa kifedha kuanza. Je, sheria ya kusimamia fedha za umma inatoa maelezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika muda huo

4. Sera za bajeti ya kitaifa na utekelezaji

  1. Kando na kushiriki katika kutayarisha bajeti, nimesikia kwamba wakenya wengine wameshiriki katika kufuatilia ikiwa fedha zimetumiwa kama zilivyopangiwa katika bajeti. Wengine wamefuatilia matumizi ya hazina ya fedha za maeneo bunge (CDF) . Je,sheria mpya zimetoa nafasi ya kufuatilia utekelzaji wa bajeti?
  2. Tumezungumzia kuhusu umma kufuatilia matumizi ya bajeti. Kando na kutazama jinsi serikali ilivyotumia fedha ilizoahidi,kuna sheria zingine ambazo lazima serikali ifuate katika makadirio ya bajeti?
  3. Nimesoma katika gazeti jinsi watu wanavyozozana kuhusu ikiwa deni la Kenya ni kubwa mno. Je,sheria ya kusimamia fedha za umma zinazungumzia kuhusu kiwango cha deni hilo au ikiwa lidhibitiwe kwa kiwango gani?
  4. Naelewa kwamba serikali hulipa madeni ya mashirika ya kiserikali. Hii ni kumaanisha kwamba mashirika ya kiserikali huenda yakawa mzigo kwa watozwa ushuru. Je, sheria ya kusimamia fedha za umma huhakikisha kwamba raia wameelezwa kuhusu madeni haya?
  5. Na misaada je? Kuna kiwango kinachokubalika cha msaada kinachoweza kupokewa na serikali, kama vile fedha kutoka kwa washirika wa miradi ya maendeleo?
  6. Naelewa kwamba,mara kwa mara, hata kama serikali imepanga vyema bajeti, matukio ambayo hayakutarajiwa husababisha bajeti hiyo kubadilishwa. Je, sheria ya kusimamia fedha za umma zinaruhusu mabadiliko hayo?

5. Serikali za ugatuzi na usambazaji wa fedha katika kaunti

  1. Nilidhani tumeelekea katika utawala wa ugatuzi, lakini mmezungumzia tu kuhusu serikali ya kitaifa. Je kaunti?
  2. Kuna hazina ya usawazishaji wa fedha ambayo hutoa fedha kwa kaunti. Inafanya kazi kivipi?
  3. Nani anayeamua kiwango cha fedha kinachotolewa kwa kaunti?
  4. Kaunti hupata fedha zao wakati gani?
  5. Kuna masharti yeyote yanayoweza kuzuia serikali kutuma fedha kwa kaunti?
  6. Ni wazi kwamba huenda serikali ya kitaifa na serikali za kaunti zikashirikiana mara kwa mara, kwa ajili ya kugawanya mapato ya fedha ya serikali. Je, sheria ya kusimamia fedha za umma inaelekeza jinsi serikali ya kitaifa na serikali za kaunti zitafanya kazi pamoja?

6. Jinsi bajeti ya kaunti inavyoundwa

  1. Nataka kujua kuhusu matayarisho ya bajeti ya kaunti na jinsi ninavyoweza kushiriki. Ndiyo sababu mlitueleza tutake kujua kuhusu sheria za kusimamia fedha za kitaifa. Basi nitashiriki kivipi na wakati gani katika matayarisho ya bajeti ya kaunti?
  2. Lazima nitoe maoni kuhusu taarifa ya mpango wa maendeleo ya kaunti itakapochapishwa kila mwezi, lakini naweza kutoa maoni yangu wakati mpango huo wa maendeleo unapotayarishwa?
  3. Hata kama nimeshiriki katika hatua ya kuandaa mipangilio, lakini ninaweza kushiririki kivipi wakati bajeti inapotayarishwa ili kuhakikisha makadirio yanashughulikia mahitaji yetu?
  4. Kwa vile ni desturi kwamba taarifa ya mikakati ya kifedha huwasilishwa baada ya taarifa ya sera za bajeti ya kitaifa, hii inamaanisha pia mapendekezo ya bajeti ya kaunti yatawasilishwa baada ya mapendekezo ya bajeti ya kitaifa?
  5. Katika ngazi ya kitaifa, kamati ya bajeti huwa na umuhimu mkuu kwa umma ambapo wao hupokea maoni yao. Kuna kamati ya bajeti katika bunge la kaunti?
  6. Je, kuna masharti kuhusu mabadiliko yanayoweza kutekelezwa katika bunge la kaunti kama ilivyo katika bunge la kitaifa?
  7. Je, kuna masharti yeyote kuhusu matumizi ya fedha katika serikali ya kaunti kama ilivyo katika serikali ya kitaifa?
  8. Je, katika serikali ya kitaifa kuna mbinu zinazotumika kubadilisha bajeti baada ya kuidhinishwa,kama vile bajeti ya ziada na hazina ya dharura. Hizi zipo katika serikali ya kaunti?
  9. Katika serikali ya kitaifa, bunge linaweza kuidhinisha matumizi ya fedha hata kama mswada wa matumizi ya fedha haujapitishwa. Haya pia hufanywa katika serikali ya kaunti?
  10. Sawa, na je kuhusu kufuatilia utekelezaji wa bajeti ya kaunti?
  11. Tulizungumzia kuhusu matakwa mapya kuhusu serikali ya kitaifa kuelezea jinsi inavyodhibiti deni la kitaifa na kulisimamia vilivyo. Na je, katika kaunti?
  12. Je, serikali za kaunti zinaweza kupokea msaada kutoka kwa washiriki wa miradi ya maendeleo?

7. Mapato na ushuru

  1. Tumezungumza kuhusu matumizi ya fedha na madeni, na je, kuhusu ushuru? Sheria ya kusimamia fedha za umma zinasema nini kuhusu ushuru katika serikali ya kitaifa?
  2. Je, sheria a kusimamia fedha za umma zinasema nini kuhusu ushuru wa kaunti?
  3. Tumezungumzia kuhusu taarifa nyingi. Naweza kupata maelezo kuhusu taarifa zote zinazopaswa kuweka wazi kwa umma katika serikali ya kitaifa na ya kaunti na kwa wakati gani?

8. Uwajibikaji

  1. Hizi zote ni sheria nzuri lakini linalonitia wasiwasi ni uwajibikaji. Kenya imekuwa na sheria nzuri tangu jadi,lakini watu hupenda kuiba fedha za umma kila wanapopata nafasi. Sheria hizi mpya zimebuni njia ya kuhakikisha maafisa wamewajibika?
  2. Ni nini kitakachofanywa ikiwa afisa mkuu wa fedha atashirikiana na waziri wa fedha kufuja fedha za umma? Nani atakayehakikisha wamewajibika?
  3. Ripoti za mkaguzi wa kitaifa wa fedha zinazotathmini uwajibikaji wa taasisi za kiserikali huwasilishwa bungeni. Ripoti hizi hutolewa kwa umma?
  4. Maafisa wa umma na taasisi za kiserikali watadhibitiwa kivipi wakifuja fedha?

9. Miji, maeneo ya mijini,utoaji huduma na maswali ya ziada

  1. Nimesikia kwamba miji na maeneo ya mjini wana mwongozo wa kutengeneza bajeti. Sheria ya kusimamia bajeti imeshughulikia swala hili?
  2. Kuna mambo yeyote tunapaswa kufahamu katika sheria ya kusimamia fedha za umma,ambayo yanaweza kuathiri mapokezi ya huduma za elimu, afya na maji?
  3. Huduma nyingi hutolewa na wahudumu wa kibinafsi kwa niaba ya serikali. Hali hii imechangia katika matumizi mabaya ya fedha. Sheria ya kusimamia fedha za umma imesema nini kuhusu maswala ya zabuni?
  4. Kila kitu kipo katika sheria hii? Mbona sheria hiyo ni ndefu na mwongozo huu ni mfupi sana?
  5. Stakabadhi husaidia, lakini kuna mtu yeyote ninayeweza kuzungumza naye ikiwa nina maswali ya ziada?

Tazama mwongozo kamili kuhusu Mambo 50 Mkenya Anapaswa Kujua Kuhusu Usimamizi wa Fedha za Umma Kuambatana na Katiba(Kiungo cha Nje) (PDF).

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/fedha-za-umma/