Ruka hadi Yaliyomo

Mimi, ……………… , naapa ya kwamba/nakubali kwa dhati kwamba kila wakati Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya; kwamba nitatekeleza wajibu wangu kwa bidii na kutekeleza kazi zangu katika afisi hiyo kwa uwezo wangu wote; na kwamba kwa wakati wowote ule nitakaohitajika, kumshauri Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa uaminifu na ukweli; kwamba nitatenda haki kwa wote bila woga, upendeleo, upendo au chuki; na kwamba sitatoa siri zozote zitakazonifikia katika shughuli zangu za kazi ama moja kwa moja au kupitia kwa yeyote. (Kama ni kiapo: Ee Mungu nisaidie).

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-3/kiapo-cha-afisi-ya-naibu-wa-rais/