Ruka hadi Yaliyomo

Mimi…………………………….., ninayeteuliwa kuwa Waziri wa Kenya, ninaapa ya kwamba/ninakubali kwa dhati kwamba nitakuwa mwaminifu wakati wowote kwa Jamhuri ya Kenya; kwamba nitaitii, nitaiheshimu na kuitetea Katiba hii ya Kenya na sheria nyingine zote za Jamhuri; kwamba nitawahudumia vyema na kwa uaminifu watu na Jamhuri ya Kenya katika Afisi ya Waziri; kwamba nitaitumikia afisi yangu kama Waziri kwa heshima na hadhi; kwamba nitakuwa mshauri wa kweli na mwaminifu kwa Rais au kwa usimamizi mwema wa masuala ya umma katika Jamhuri ya Kenya; kwamba sitatoa siri zozote zitakazonifikia katika shughuli zangu za kazi ama moja kwa moja aukupitia kwa yeyote isipokuwa pale inapohitajika katika utekelezaji wa kazi zangu za uwaziri; na kwamba nitatekeleza majukumu ya afisi yangu kwa uangalifu na kwa uwezo wangu. ( Kama ni kiapo –Ee Mungu nisaidie).

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-3/kiapo-cha-afisi-ya-waziri/