Ruka hadi Yaliyomo

Mimi, ……………………, nikiwa ninahitajika kuchukua wajibu wa katibu wa Baraza la Mawaziri/ Katibu Mkuu ninaapa ya kwamba/ninakubali kwa dhati kwamba, isipokuwa kwa idhini ya Rais, sitafichua habari za shughuli yoyote, taratibu au nyaraka za Baraza la Mawaziri ninazohitaji kuzihifadhi kwa siri, kwa njia ya moja kwa moja au kupitia kwa yeyote, isipokuwa pale ambapo zinahitajika kutokana na shughuli zangu za kazi kama Katibu wa Baraza la Mawaziri/Katibu Mkuu. (Kama ni kiapo:-Ee Mungu nisaidie).

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-3/kiapo-cha-katibu-wa-baraza-la-mawaziri-na-katibu-mkuu/