Ruka hadi Yaliyomo

Mimi, ……………. , nikifahamu kuwa jukumu muhimu ninalochukua kama Rais /Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, naapa/nakiri kwa dhati kuwa nitakuwa mwaminifu kwa Jamjuri ya Kenya; kwamba nitafuata, kuhifadhi, kutetea, Katiba ya Kenya, kulingana na sheria iliyowekwa, na sheria nyingie zote za Jamhuri, na kwamba nitalinda na kutetea uhuru, uadilifu na heshima ya watu wa Kenya. ( Kama ni kiapo: Ee Mungu nisaidie)

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-3/kiapo-cha-rais-kaimu-rais-na-naibu-rais/