Ruka hadi Yaliyomo

Mimi,……………………, nikiwa nimechaguliwa mwachama wa Seneti/Baraza Kuu la Kitaifa ninaapa (Kwa jina la Mwenyezi Mungu) (ninathibitisha kwa dhati) kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa Watu na Jamhuri ya Kenya; kwamba nitatii, kuheshimu, kutetea, kulinda na kuhifadhi Katiba ya Jamhuri ya Kenya; na kwamba nitatekeleza majukumu yangu ya ubunge kwa uaminifu na uangalifu. (Ee Mungu nisaidie).

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-3/kiapo-cha-wabunge/