(Mamlaka na kazi za serikali ya kitaifa—)
- Mashauri ya kigeni, sera ya kigeni, na biashara ya kimataifa.
- Matumizi ya maji ya kimataifa na rasilimali za maji.
- Uhamiaji na uraia.
- Uhusiano kati ya dini na serikali.
- Sera ya lugha na ukuzaji wa lugha rasmi na lugha za kiasili.
- Ulinzi wa kitaifa na matumizi ya huduma za ulinzi za kitaifa..
- Huduma za polisi , pamoja na—
(a) Kuweka viwango vya kuajiri, mafunzo kwa polisi na matumizi ya huduma za polisi;
(b) Sheria ya jinai; na
(c) Huduma za Marekebisho. - Mahakama.
- Sera ya kitaifa ya uchumi na mipango.
- Sera ya fedha, sarafu, benki (pamoja na benki kuu) kuanzishwa pamoja na usimamizi wa shughuli za benki, bima na mashirika ya kifedha.
- Takwimu za kitaifa na data kuhusu idadi ya watu, uchumi na jamii kwa jumla.
- Haki miliki
- Viwango vya utendakazi.
- Ulinzi wa watumiaji, pamoja na viwango vya usalama wa kijamii na mipango ya kitaalamu ya kustaafu.
- Sera ya Elimu, viwango, Mitalaa, mitihani, na utoaji wa hati za vyuo vikuu.
- Vyuo Vikuu, taasisi za mafunzo ya kati na taasisi nyingine za utafiti na masomo ya juu na shule za msingi, elimu maalumu, shule za upili na vyuo vya elimu maalumu.
- Ukuzaji wa michezo na elimu ya michezo.
- Uchukuzi na mawasiliano, pamoja na, hasa—
(a) Usafiri wa barabara;
(b) Ujenzi na matumizi ya barabara kuu za kitaifa;
(c) Viwango vya ujenzi na uhifadhi wa barabara zingine za kaunti;
(d) Reli;
(e) Mifereji ya mabomba;
(f) Usafiri wa baharini;
(g) vyombo vya anga vinavyotumiwa na raia;
(h) Usafiri wa angani;
(i) Huduma za posta;
(j) Mawasiliano ya simu, redio na runinga na;
(k) matangazo ya redio na runinga. - Huduma ya kitaifa ya kazi za umma.
- Sera ya nyumba.
- Kanuni za kijumla za mipango ya ardhi na ushirikishaji wa mipango na kaunti.
- Uhifadhi wa mazingira na maliasili kwa mpango wa kuanzisha mfumo wa maendeleo endelevu, pamoja na, hasa—
(a) Uvuvi, usasi na ukusanyaji;
(b) Ulinzi wa wanyama wa kufugwa na wanyama pori;
(c) Uhifadhi wa maji, kuhifadhi wa mabaki ya maji, uhandisi unaohusu maji na usalama wa mabwawa; na
(d) Sera ya kawi - Hospitali za Kitaifa.
- Usimamizi wa majanga.
- Minara ya zamani ya kihistoria yenye umuhimu wa kitaifa.
- Chaguzi za kitaifa.
- Sera ya Afya.
- Sera ya Kilimo.
- sera ya utatibu wa mifugo.
- Sera ya kawi pamoja na nguvu za umeme, mtandao wa gesi, na usimamiaji wa kawi.
- Ujenzi wa utendakazi na usaidizi wa kiufundi katika kaunti
- Uwekezaji wa umma.
- Uwekaji dau wa kitaifa, makasino na aina mbalimbali za uchezaji kamari.
- Sera ya utalii na maendeleo.