Ruka hadi Yaliyomo

Sheria Zitakazotungwa na Bunge

Sura na Kifungu Muda Uliowekwa
SURA YA PILI – JAMHURI
Sheria kuhusu utamaduni (Kifungu cha 11 (3)) Miaka Mitano
SURA YA TATU – URAIA
Sheria kuhusu uraia (Kifungu cha 18) Mwaka Mmoja
SURA YA NNE – SHERIA YA HAKI
Uhuru wa vyombo vya habari (Kifungu cha 34) Miaka Mitatu
Familia (Kifungu cha 45) Miaka Mitano
Ulinzi kwa watumiaji bidhaa (Kifungu cha 46 Miaka Minne
Haki katika mambo ya kiutawala (Kifungu cha 47) Miaka Minne
Haki ya kusikilizwa (Kifungu cha 50) Miaka Minne
Haki ya watu walio kizuizini, walioshikwa au waliofungiwa (Kifungu cha 51) Miaka Minne
Tume ya kitaifa ya Haki za Binadamu na Usawa ya Kenya (Kifungu cha 59) Mwaka Mmoja
SURA YA TANO – ARDHI NA MAZINGIRA
Ardhi ya jamii (Kifungu cha 63) Miaka Mitano
Usimamizi wa matumizi ya ardhi na mali (Kifungu cha 66) Miaka Mitano
Sheria ya ardhi (Kifungu cha 68) Miezi 18
Maafikiano kuhusu maliasili (Kifungu cha 71) Miaka Mitano
Sheria kuhusu mazingira (Kifungu cha 72) Miaka Minne
SURA YA SITA – UONGOZI NA MAADILI
Tume ya Maadili na kupambana na Ufisadi (Kifungu cha 79) Mwaka Mmoja
Sheria ya uongozi (Kifungu cha 80) Miaka Miwili
SURA YA SABA – UWAKILISHI WA WATU
Sheria ya uchaguzi (Kifungu cha 82) Mwaka Mmoja
Mizozo ya kiuchaguzi (Kifungu cha 87) Mwaka Mmoja
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (Kifungu cha 88)) Mwaka Mmoja
Sheria ya vyama vya kisiasa (Kifungu cha 92) Mwaka Mmoja
SURA YA NANE – BUNGE
Kuimarisha uwakilishi wa jamii zilizotengwa (Kifungu cha 100) Miaka Mitano
Kuachwa wazi kwa afisi ya mbunge (Kifungu cha 103) Mwaka Mmoja
Haki ya kumwondoa mbunge (Kifungu cha 104) Miaka Miwili
Uamuzi wa masuala ya uanachama wa Bunge (Kifungu cha 105) Miaka Miwili
Haki ya kupeleka malalamiko kwa Bunge (Kifungu cha 119) Miaka Miwili
SURA YA TISA – MAMLAKA YA UTAWALA
Mamlaka ya kusamehe (Kifungu cha 133) Mwaka Mmoja
Kuchukua mamlaka ya afisi ya Rais (Kifungu cha 141) Miaka Miwili
SURA YA KUMI - MAHAKAMA
Utaratibu wa mahakama (Kifungu cha 162) Mwaka Mmoja
Kuondolewa afisini (Kifungu cha 168) Mwaka Mmoja
Mfuko wa Mahakama (Kifungu cha 173) Miaka Miwili
Ukaguzi wa majaji na mahakimu (Mpangilio wa sita sehemu ya 23) Mwaka Mmoja
SURA YA KUMI NA MOJA – SERIKALI YA UGATUZI
Spika wa baraza la kaunti (Kifungu cha 178) Mwaka Mmoja
Sehemu za miji na majiji (Kifungu cha 183) Mwaka Mmoja
Usaidizi kwa serikali za kaunti (Kifungu cha 190) Miaka Mitatu
Kuondolewa kwa gavana wa kaunti (Kifungu cha 181) Miezi 18
Kuachwa wazi kwa afisi ya mwanachama wa baraza la kaunti (Kifungu cha 194) Miezi 18
Kushiriki kwa umma na mamlaka ya baraza la kaunti, mapendeleo na kinga Miaka Mitatu
Usawa wa kijinsia na tofauti za kijamii katika baraza la kaunti (Kifungu cha 197) Miaka Mitatu
Sheria ya kuanza kutumiwa kwa Sura ya kumi na moja (Kifungu cha 200 na mpangilio wa sita sehemu ya 15) Miezi 18
SURA YA KUMI NA MBILI – FEDHA ZA UMMA
Mapato ya pesa kwa serikali za kaunti (Kifungu cha 207) Miezi 18
Mfuko wa Dharura (Kifungu cha 208) Mwaka Mmoja
Udhamini wa mikopo na serikali ya kitaifa (Kifungu cha 213) Mwaka Mmoja
Usimamizi wa pesa (Kifungu cha 225) Miaka Miwili
Mahesabu na ukaguzi wa mashirika ya umma (Kifungu cha 226) Miaka Minne
Ununuzi wa bidhaa na huduma za umma (Kifungu cha 227) Miaka Minne
SURA YA KUMI NA TATU – HUDUMA ZA UMMA
Maadili na kanuni za huduma za umma (Kifungu cha 232) Miaka Minne
SURA YA KUMI NA NNE – USALAMA WA KITAIFA
Idara za usalama wa kitaifa (Kifungu cha 239) Miaka Miwili
Utawala wa huduma ya polisi ya kitaifa (Kifungu cha 245) Miaka Miwili
KAULI YA JUMLA
Sheria nyingine yoyote itakayohitajiwa na Katiba hii Miaka Mitano
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-5/sheria-zitakazotungwa-na-bunge/