Ruka hadi Yaliyomo

(1) Hadi pale Bunge litakapopitisha Sheria inayotarajiwa katika Vifungu vya 15 na 18, sehemu ya 93 ya Katiba ya awali inaendelea kutumika.

(2) Sehemu za 30 hadi 40, 43 hadi 46, 48 hadi 58 za Katiba ya awali, masharti ya Katiba ya awali kuhusu mamlaka ya serikali, na Mwafaka wa Kitaifa na Sheria ya Maridhiano, ya mwaka wa 2008 (Na. 4 ya 2008) zitaendelea kutumika hadi uchaguzi mkuu wa kwanza utakapofanywa chini ya Katiba hii, lakini masharti ya Katiba hii kuhusu mfumo wa uchaguzi, ustahili wa mtu katika uchaguzi na utaratibu wa uchaguzi utatumika katika uchaguzi huo.

(3) Hadi pale ambapo Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa inayorejelewa katikaKifungu cha 246 imeundwa, sehemu ya 108 (2) ya Katiba ya awali itatumika katika uteuzi wa kazi, masuala ya nidhamu na kuachishwa kazi kwa watu katika Huduma za Polisi za Kitaifa.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-6/sehemu-1/masharti-ya-katiba-ya-awali/