(1) Sheria zote zinazotumika kabla ya tarehe ya kuanza kutekelezwa kwa Katiba hii zitaendelea kuwepo na zitafanyiwa marekebisho muhimu ili ziweze kuafikiana na Katiba hii.
(2) Iwapo, kwa mujibu wa suala lolote–
- (a) Sheria iliyokuwa ikitumika mara tu kabla ya tarehe ya kutekelezwa inaipa jukumu idara fulani ya serikali au afisi ya umma; au
- (b) Sharti la Katiba hii linalotumika linaipa majukumu idara tofauti ya serikali au afisa wa umma,
Masharti ya Katiba hii ndiyo yatakayopewa umuhimu.