Ruka hadi Yaliyomo

(1) Watu wanaoshikilia mamlaka ya Rais na Waziri Mkuu, kabla tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii, wataendelea kuhudumu kama Rais na Waziri Mkuu mtawalia, kwa mujibu wa Katiba ya awali katika Sheria ya mwaka wa 2008 ya Muafaka wa Kitaifa na Maridhiano hadi uchaguzi mkuu wa kwanza ufanyike chini ya Katiba hii, au waondoke afisini kwa mujibu wa Katiba ya awali na Muafaka wa Kitaifa na Maridhiano.

(2) Watu wanaoshikilia afisi ya Makamu wa Rais na Naibu-Waziri Mkuu au wanaoshikilia wadhifa katika Baraza la Mawaziri au Waziri Msaidizi mara tu kabla ya tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii, wataendelea kuhudumu kwa mujibu wa Katiba ya awali mpaka uchaguzi mkuu wa kwanza ufanywe chini ya Katiba hii, ila tu waondoke au kuondolewa afisini kwa mujibu wa Katiba ya awali na Sheria ya mwaka wa 2008 ya Muafaka wa Kitaifa na Mariadhiano.

(3) Mtu aliyechaguliwa Rais kabla ya tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii hatagombea uchaguzi wa urais chini ya Katiba hii.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-6/sehemu-3/mamlaka-makuu-ya-utawala/