(1) Katika mwaka mmoja baada ya tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii, Bunge litatunga sheria itakayotekelezwa licha ya Kifungu cha 160, 167 na 168, ambayo itaweka mikakati na utaratibu wa kuchunguza, katika muda utakaoamuliwa katika sheria hiyo, ustahili wa majaji na mahakimu wote waliokuwa afisini tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hiyo kuendelea kuhudumu kwa mujibu wa maadili na kanuni zilizo katika Vifungu vya 10 na 159.
(2) Kuondolewa au utaratibu utakaopelekea kuondolewa kwa jaji kutoka afisini kwa misingi ya utekelezaji wa sheria inayorejelewa katika ibara ndogo ya (1) hakutapingwa au kuchunguzwa upya, na mahakama yoyote.