Ruka hadi Yaliyomo

Raia wa Kenya ni raia kwa kuzaliwa iwapo–

  • (1) amepata uraia chini ya kifungu cha 87 au 88 (1) cha Katiba ya awali; au
  • (2) angepata uraia kama kifungu cha 87 (2) kingesomwa:
    “Kila mtu ambaye alizaliwa nje ya Kenya, na mnamo tarehe 11-Disemba, 1963 ni raia wa Uingereza na Koloni zake au mtu aliyepata ulinzi wa Uingereza atakuwa, iwapo mamake au babake atakuwa , au angekuwa lakini kwa sababu ya kifo cha mmoja au wote wamekuwa, raia wa Kenya kwa sababu ya ibara ndogo ya (1), atakuwa raia wa Kenya mnamo tarehe 12 Disemba, 1963.”
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-6/sehemu-6/masuala-ya-ziada/uraia-kwa-kuzaliwa/