Ruka hadi Yaliyomo

(1) Tume ya Mipaka iliyobuniwa chini ya Katiba ya awali itaendelea kuhudumu kama ilivyoundwa katika Katiba hiyo na kwa masharti ya ibara za 41 B na 41 C lakini–

  • (a) Haitaweka mipaka ya kaunti zilizoundwa chini ya Katiba hii;
  • (b) Itaweka mipaka ya maeneo bunge na wadi ikitumia vigezo vilivyotajwa katika Katiba hii; na
  • (c) Wanachama wa Tume hii wataongozwa na Sura ya Saba ya Katiba hii.

(2) Yanayohitajika katika Kifungu cha 89 (2) kwamba uchunguzi upya wa mipaka ya maeneo bunge na wadi ukamilishwe angalau miezi kumi na miwili kabla ya uchaguzi mkuu hayatahusiana na uchunguzi upya wa mipaka kabla ya uchaguzi wa kwanza chini ya Katiba hii.

(3) Tume ya Mipaka itahakikisha kuwa uchunguzi upya wa kwanza wa mipaka ya maeneo bunge chini ya Katiba hii hautasababisha kupotea kwa eneo bunge lililokuwepo wakati wa tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-6/sehemu-6/tume-huru-ya-muda-ya-mipaka/