Ruka hadi Yaliyomo

(1) Tume ya Utekelezaji wa Katiba na Tume ya Ugavi wa Mapato zitaundwa katika siku tisini baada ya tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii.

(2) Tume ya Mishahara na Kuzawidi itaundwa katika miezi tisa baada ya tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii.

(3) Hadi pale ambapo sheria inayorejelewa katika Kifungu cha 256 itekelezwe, watu watakaoteuliwa kama wanachama au mwenyekiti wa Tume ya Mishahara na Kuzawidi watateuliwa na Rais, kutegemea Sheria ya Muafaka wa Kitaifa na Maridhiano, na baada ya kushauriana na Waziri Mkuu na kuidhinishwa na Baraza Kuu la Kitaifa.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/mipangilio/mpangilio-6/sehemu-6/tume-za-kikatiba/