Ruka hadi Yaliyomo

(1) Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya na yanaweza kutekelezwa tu kulingana na Katiba hii.

(2) Wananchi watatekeleza mamlaka yao kwa njia ya moja kwa moja au kupitia kwawawakilishi wao waliochaguliwa kidemokrasia.

(3) Mamlaka ya wananchi katika Katiba hii yamepewa idara zifuatazo za Serikali, ambazo zitatekeleza majukumu yao kulingana na Katiba hii–-

  • (a) Bunge na mabaraza ya kutunga sheria katika Serikali za Kaunti;
  • (b) Serikali ya kitaifa na mifumo ya Serikali za Kaunti; na
  • (c) Idara ya mahakama na tume zingine huru.

(4) mamlaka ya wananchi yanatekelezwa katika-

  • (a) kiwango cha kitaifa; na
  • (b) kiwango cha kaunti.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-1/kifungu-1/mamlaka-ya-watu/