(1) Mamlaka ya Mahakama yanatokana na watu, yanajikita katika mahakama na mahakama maalum zinazobuniwa kulingana na Katiba hii.
(2) Katika kutekeleza majukumu ya kimahakama, mahakama na mahakama maalum zitaongozwa na kanuni zifuatazo–
- (a) haki itatendwa kwa kila mtu bila kuzingatia hadhi;
- (b) Haki haitacheleweshwa;
- (c) njia m’badala za kusuluhisha kesi zikiwemo msamaha, mashauriano, na maridhiano na njia za kitamaduni za kusuluhisha migogoro zitaimarishwa, kwa mujibu wa ibara ya (3);
- (d) haki itatolewa kwa kuzingatia matatizo yaliyopo ya utaratibu wa kitaalamu; na
- (e) lengo na kanuni za Katiba hii zitatunzwa na kuendelezwa.
(3) Mbinu za kitamaduni za utatuaji wa migogoro hazitatumiwa kwa njia ambayo–
- (a) itakiuka Sheria za Haki;
- (b) itagongana na haki na maadili au kusababisha matokeo yatakayogongana na haki na maadili;
- (c) haiambatani na Katiba hii au sheria yoyote iliyoandikwa.