(1) Katika utekelezaji wa mamlaka ya mahakama, Mahakama kama ilivyoundwa chini ya kifungu cha 161, itazingatia Katiba hii pamoja na sheria na haitadhibitiwa wala kuelekezwa na mtu yeyote mwingine au halmashauri.
(2) Afisi ya jaji wa mahakama ya Mamlaka Kuu haitafutiliwa mbali wakati ambapo kuna afisa anayeshikilia wadhifa huo.
(3) Mishahara na marupurupu yanayofaa kulipwa, au kuhusiana na, majaji yatatoka kwa Mfuko wa Jumla wa Serikali.
(4) Kulingana na Kifungu cha 168 (6), mishahara na marupurupu inayofaa kulipwa, au kuhusiana na majaji haitabadilishwa kwa njia itakayowaathiri, na marupurupu ya kustaafu ya jaji hayatabadilishwa ili kumuathiri jaji mstaafu katika maisha yake ya uhai.
(5) Mwanachama wa mahakama hatawajibika katika hatua au kesi kuhusiana na chochote watakachofanya au watakachokosa kufanya kwa nia njema katika utendaji kazi wa kisheria kwa kutekeleza majukumu ya mahakama.