(1) Mahakama inahusisha majaji wa mahakama za mamlaka ya juu, mahakimu na maafisa wengine wa idara ya Mahakama.
(2) Kutabuniwa afisi ya–
- (a) Jaji Mkuu, atakayekuwa Mkuu wa Mahakama;
- (b) Naibu Jaji Mkuu, atakayekuwa Naibu Mkuu wa Mahakama;
- (c) Msajili Mkuu wa Idara ya Mahakama ambaye ni msimamizi mkuu wa kiutawala na afisa wa uhasibu wa Idara ya Mahakama.
(3) Tume ya Huduma za Mahakama inaweza kuunda afisi nyingine za masjala ikiwa pana haja ya kufanya hivyo.