(1) Jaji atastaafu kutoka afisini atakapofikisha umri wa miaka sabini, lakini anaweza kuamua kustaafu wakati wowote baada ya kufikisha miaka sitini na tano.
(2) Jaji Mkuu atahudumu afisini kwa jumla ya miaka kumi au hadi wakati wa kustaafu chini ya Ibara ya (1), kutegemea itakayofika mwanzo.
(3) Iwapo kipindi cha Jaji Mkuu kuhudumu kitakamilika kabla ya kufikisha umri wa kustaafu chini ya ibara ya (1) , Jaji Mkuu anaweza kuendelea kuhudumu kama jaji wa Mahakama ya Juu.
(4) Iwapo, wakati wa kukamilika kwa kipindi cha kuhudumu cha Jaji Mkuu, Jaji huyu ataamua kuendelea kuhudumu mahakamani chini ya ibara ya (3), mtu atakayeteuliwa kama Jaji Mkuu atateuliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 166(1) ingawa uteuzi huo utasababisha kuwepo kwa idadi inayozidi idadi inayokubalika ya majaji wa Mahakama ya Juu.
(5) Jaji Mkuu na jaji mwingine yeyote anaweza kujiuzulu kutoka afisini kwa kuandika barua kwa Rais.