Ruka hadi Yaliyomo

(1) Mahakama saidizi ni–

  • (a) Mahakama za Mahakimu;
  • (b) Mahakama za Kadhi;
  • (c) Mahakama ya Kijeshi; na
  • (d) Mahakama yoyote nyingine au mahakama maalum kama inavyoweza kubuniwa kwa Sheria ya Bunge, isipokuwa mahakama zilizobuniwa kwa mujibu wa kifungu cha 162 (2).

(2) Bunge, kwa njia ya sheria litatoa mipaka, mamlaka na majukumu kwa mahakama ambazo zilizobuniwa chini ya ibara ya (1).

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-10/sehemu-3/kifungu-169/mahakama-ndogo/