(1) Tume ya Huduma za Mahakama imeundwa.
(2) Tume hii inajumuisha–
- (a) Jaji Mkuu, atakayekuwa mwenyekiti wa Tume;
- (b) Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu aliyeteuliwa na majaji wa Mahakama ya Juu;
- (c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa aliyeteuliwa na majaji wa mahakama ya Rufaa;
- (d) Jaji mmoja wa Mahakama Kuu na hakimu mmoja, mwanamke mmoja na mwanamme mmoja, walioteuliwa na wanachama wa muungano wa majaji na mahakimu;
- (e) Mwanasheria Mkuu;
- (f) Mawakili wawili, mwanamke mmoja na mwanamme mmoja, kila mmoja awe na tajriba isiyopungua miaka kumi na tano, walioteuliwa na chama kilichokubaliwa kisheria kusimamia taaluma ya uwakili;
- (g) mtu mmoja aliyeteuliwa na Tume ya Huduma ya Umma; na
- (h) mwanamke mmoja na mwanamme mmoja kuwakilisha umma,wasiokuwa wanasheria, watakaoteuliwa na Rais kwa idhini ya Baraza la Kitaifa.
(4) Mkuu wa Masjala ya Mahakama atakuwa Katibu wa Tume.
(5) Wanachama wa Tume, isipokuwa Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu watahudumu kwenye afisi, mradi tu wawe wamehitimu, kwa kipindi cha miaka mitano na wataweza kuteuliwa kuhudumu zaidi kwa kipindi kingine cha miaka mitano na cha mwisho.