Serikali za kaunti zilizobuniwa chini ya Katiba hii zitazingatia kanuni zifuatazo–
- (a) Serikali za kaunti zitazingatia misingi ya kidemokrasia na utengano wa mamlaka.
- (b) Serikali za kaunti sharti ziwe na njia za kuaminika za kuzalisha mapato ili kuziwezesha kuendesha shughuli zao na kutoa huduma kwa njia bora; na
- (c) isiyo zaidi ya theluthi mbili ya wanachama wawakilishi wa taasisi za umma katika Serikali za kaunti watakuwa wa jinsia moja.