(1) Kila baraza la kaunti litakuwa na spika aliyechaguliwa na baraza la kaunti kutoka kwa watu wasio wanachama wa baraza hilo.
(2) Kinara wa kikao cha baraza la kaunti atakuwa–
- (a) spika wa baraza hilo; au
- (b) wakati spika hayupo, mwanachama mmoja aliyeteuliwa na baraza hilo.
(3) Baraza litatunga sheria itakayoruhusu kuchaguliwa na kuondolewa afisini kwa maspika wa mabaraza ya kaunti.