Ruka hadi Yaliyomo

(1) Afisi ya gavana wa kaunti itaachwa wazi iwapo anayeshikilia afisi hiyo–

  • (a) atafariki;
  • (b) atajiuzulu kwa kumwandikia spika wa baraza la kaunti;
  • (c) hafai kwa mujibu wa kifungu cha 180 (2);
  • (d) atapokea kifungo kwa kosa ambalo adhabu yake ni kufungwa gerezani kwa miezi isiyopungua kumi na miwili;
  • (e) ataondolewa afisini kwa mujibu wa katiba hii.

(2) Iwapo afisi ya gavana wa kaunti itakuwa wazi, naibu gavana atatekeleza majukumu ya gavana kwa kipindi kilichosalia cha gavana kuhudumu.

(3) Iwapo mtu ataikalia afisi kwa mujibu wa ibara ya (2), kwa minajili ya kifungu cha 180(7) , mtu huyo atachukuliwa kuwa–

  • (a) amehudumu kipindi kizima cha gavana wa kaunti iwapo, kufikia tarehe mtu huyo alipoingia afisi hiyo, zaidi ya miaka miwili na nusu imesalia kabla ya tarehe ya uchaguzi mwingine ilivyo kawaida chini ya kifungu cha 180 (1); au
  • (b) hajahudumu afisini kama gavana wa kaunti iwapo ni hali nyingine yoyote.

(4) Iwapo nafasi itatokea katika afisi ya gavana wa kaunti na ile ya naibu gavana wa kaunti au iwapo naibu gavana wa kaunti hawezi kuishikilia kwa muda, spika wa baraza la kaunti atashikilia afisi hiyo kwa muda.

(5) Iwapo nafasi itatokea katika hali inayotjwa katika ibara ya (4), uchaguzi wa gavana wa kaunti utafanywa kati ya siku sitini baada ya tarehe ya spika kuanza kushikilia afisi hiyo.

(6) Mtu atakeyechukua nafasi ya kuhudumu katika afisi ya gavana wa kaunti chini ya kifungu hiki, ila tu aondolewe afisini kwa mujibu wa Katiba hii, ataendelea kuhudumu hadi gavana mwingine atakapochaguliwa wakati wa uchaguzi unaofuata kwa mujibu wa kifungu cha 180 (1).

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-11/sehemu-2/kifungu-182/nafasi-katika-afisi-ya-gavana/