(1) Kamati kuu ya kaunti ina majukumu yafuatayo–
- (a) utekelezaji wa sheria za bunge la kaunti;
- (b) utekelezaji, katika kaunti , sheria za taifa inavyohitajika kisheria;
- (c) kusimamia shughuli za utawala wa kaunti na idara zake; na
- (d) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Katiba hii na sheria ya nchi.
(2) Kamati kuu ya kaunti inaweza kuandaa sheria iliyopendekezwa na kuziwasilisha kwa bunge la kaunti.
(3) Kamati kuu ya kaunti itatoa ripoti kamili za mara kwa mara kwa baraza la kaunti kuhusu masuala yaliyo chini ya udhibiti wa kamati hiyo.