Ruka hadi Yaliyomo

(1) Sheria ya Kitaifa itaidhinisha utawala na usimamizi wa maeneo ya mijini na majiji na hususan ita–

  • (a) buni vigezo vya kuainisha maeneo kama miji na majiji;
  • (b) buni kanuni za utawala na usimamizi wa maeneo ya mijini na majiji; na
  • (c) ruhusu ushiriki wa umma katika utawala wa maeneo ya mijini na majiji.

(2) Sheria ya kitaifa inyorejelewa katika Ibara ya (1) inaweza kujumuisha njia za kutambua kategoria mbalimbali za maeneo ya mijini na majiji, na utawala wao.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-11/sehemu-2/kifungu-184/miji-na-majiji/