(1) Mipaka ya kaunti inaweza kubadilishwa kwa pendekezo tu–
- (a) lililopendekezwa na Tume huru iliyobuniwa na bunge kwa lengo hilo; na
- (b) liliyoidhinishwa na–
- (i) Baraza la Kitaifa likiungwa mkono na wabunge wasiopungua thuluthi mbili wa bunge hilo; na
- (ii) seneti ikiungwa mkono na angalau wawakilishi wa kaunti wasiopungua thuluthi mbili ya ujumbe wa kaunti.
(2) Mipaka ya kaunti inaweza kubadilishwa kwa kuzingatia–
- (a) wingi wa watu na uongezekaji wao;
- (b) miundomsingi na uhalisia wao;
- (c) mshikamano wa kihistoria na misingi ya kitamaduni;
- (d) gharama za usimamizi;
- (e) maoni ya jamii zilizoathirika;
- (f) malengo ya ugatuzi wa Serikali; na
- (g) sifa za kijiografia.