Ruka hadi Yaliyomo

(1) Serikali katika viwango vyovyote–

  • (a) itaendesha na kutumia mamlaka yake ikiheshimu utekelezaji na heshima za taasisi nyinginezo za viwango vingine za Serikali na kuheshimu hadhi ya kikatiba na taasisi za serikali katika viwango vingine, na kwa serikali ya kaunti, katika kiwango cha kaunti;
  • (b) kusaidia, kushirikiana na kushauriana na Serikali katika viwango vyote vifaavyo, kutekeleza sheria katika viwango vyote vya Serikali; na
  • (c) kushauriana na Serikali katika ngazi tofauti tofauti kwa minajili ya kubadilishana mawazo, kusimamia sera na utawala, huku uwezo ukikuzwa.

(2) Serikali katika viwango tofauti na serikali tofauti za kaunti zitashirikiana katika kutekeleza majukumu na mamlaka yao, kwa lengo hilo, zitaunda muungano wa kamati na mamlaka.

(3) Katika kutofautiana kokote kule kwa Serikali, Serikali inayohusika itafanya kila jitihada kutatua mzozo huo ikizingatia taratibu za kisheria kama zilivyo katika sheria ya taifa.

(4) Sheria ya kitaifa itatoa mwongozo na taratibu za kutatua mizozo kati ya Serikali kwa mbinu m’badala za kutatua mizozo zikiwemo kushauriana, kupatanisha na kusuluhisha.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-11/sehemu-5/kifungu-189/ushirikiano-wa-serikali/