(1) Rais anaweza kusimamisha serikali ya kaunti kwa muda–
- (a) wakati wa dharura inayotokana na mizozo ya ndani au vita; au
- (b) wakati wa hali za kipekee zinazohitaji kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo.
(2) Serikali ya kaunti haitasimamishwa kwa muda kulingana na ibara ya (1) (b) hadi tume huru ifanye uchunguzi wa mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake, Rais wa taifa aridhike kwamba mashtaka ni ya haki na seneti imeyaidhinisha.
(3) wakati wa kusimamishwa kwa muda katika kifungu hiki, mipango itafanywa ya kutekeleza majukumu ya kaunti kulingana na Sheria za Bunge.
(4) Seneti yaweza, wakati wowote, kufutilia mbali kusimamishwa huko kwa muda.
(5) kusimamishwa kwa muda katika kifungu hiki hakuwezi kuwa kwa zaidi ya siku tisini.
(6) Muda uliotengwa kulingana na Ibara ya (5) unapomalizika uchaguzi wa Serikali mwafaka ya kaunti utafanyika.