Ruka hadi Yaliyomo

(1) Afisi ya mbunge wa baraza la kaunti huwa wazi kutokana na–

  • (a) iwapo mbunge atafariki;
  • (b) kama mbunge atakosa vikao vinane vya bunge bila idhini iliyoandikwa kwa spika wa bunge, na hawezi kutoa sababu za kutosha za kutohudhuria vikao hivyo;
  • (c) kama mtu huyo ataondolewa afisini kwa mujibu wa Katiba hii au kwa mujibu wa sheria ya kifungu cha 80.
  • (d) mbunge akijiuzulu kwa kumwandikia spika wa bunge;
  • (e) iwapo baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge–
    • (i) kama mwanachama wa chama cha kisiasa atajiuzulu, ama ikichukuliwa amejiuzulu kutoka kwa chama kwa mujibu wa sheria inayotajwa katika Ibara ya (2); au
    • (ii) baada ya kuchaguliwa bungeni kama mgombea huru, anajiunga na chama cha kisiasa
  • (f) kukamilika kwa kipindi cha bunge; au
  • (g) kama mwanachama ataondolewa afisini kwa misingi ya uchaguzi ilivyowekwa katika Kifungu cha 193 (2).

(2) Bunge litatunga sheria itakayoonyesha hali ambapo mwanachama wa chama cha kisiasa, atachukuliwa kuwa amejiuzulu kutoka kwa chama, kwa mujibu wa Ibara ya (1) (e).

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-11/sehemu-7/kifungu-194/kuondoka-afisini-baraza-la-kaunti/