Ruka hadi Yaliyomo

(1) Baraza la kaunti ama kamati yake yoyote, lina uwezo wa kumwita mtu yeyote mbele yake ili kutoa ushahidi au habari zinazotakikana.

(2) Kwa sababu ya ibara ya (1), baraza lina mamlaka sawa na Mahakama kuu ya–

  • (a) kuhimiza mashahidi kuhudhuria na kuwahoji baada ya kula kiapo, kukiri au hali nyingine;
  • (b) kuwalazimisha mashahidi kuwasilisha nyaraka muhimu;
  • (c) kutafuta idhini ya kuwahoji mashahidi ng’ambo.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-11/sehemu-7/kifungu-195/baraza-la-kaunti-kuita-mashahidi/