(1) Baraza la kaunti–
- (a) litaendesha shughuli zake kwa uwazi, na kufanya vikao vyake na vile vya kamati zake mbele ya umma; na
- (b) kuhimiza watu kushiriki katika kutunga sheria na katika shughuli nyingine za baraza na kamati zake.
(2) Baraza la kaunti halitawaacha nje watu, au vyombo vya habari, katika kikao chochote ila katika hali ambapo spika wa bunge ametoa uamuzi na sababu za kutosha za kufanya hivyo.
(3) Baraza litatunga sheria itakayoonyesha mamlaka, haki, na kinga ya mabaraza ya kaunti, jamii na wanachama wake.