Ruka hadi Yaliyomo

Kifungu 197. Usawa na Tofauti za Kijinsia Katika Baraza la Kaunti

(1) Wanachama wa baraza lolote la kaunti au wa kamati ya mamlaka kuu ya kaunti, wasiwe zaidi ya thuluthi mbili katika jinsia moja.

(2) Bunge litatunga sheria–

  • (a) kuhahakikisha kwamba tofauti za kijamii na za kitamaduni katika nchi zinaangaziwa kwenye mabaraza na kamati za mamlaka kuu za kaunti ; na
  • (b) kuweka mikakati ya kuwalinda walio wachache katika kaunti hizo.