Ruka hadi Yaliyomo

(1) Bunge litatunga sheria katika masuala yote muhimu au ya lazima kuidhinisha utekelazaji wa Sura hii.

(2) Hasa, sheria inaweza kubuniwa ili iangazie–

  • (a) usimamizi wa mji mkuu, majiji mengine na miji mingine;
  • (b) kuhamishwa kwa majukumu na mamlaka kutoka kwa kiwango kimoja cha Serikali hadi kingine, pamoja na kuhamisha uwezo wa kutunga sheria kutoka kwa Serikali ya kitaifa hadi Serikali za kaunti;
  • (c) taratibu za uchaguzi ama uteuzi wa watu, na kuwatoa mamlakani katika Serikali za kaunti, pamoja na kuhitimu kwa wapiga kura na wagombeaji wa viti.
  • (d) taratibu za mabaraza na kamati kuu pamoja na uenyekiti, mfululizo wa mikutano, uhudhuriaji na upigaji kura; na
  • (e) kusimamishwa kwa muda kwa mabaraza na kamati kuu.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-11/sehemu-7/kifungu-200/sheria-kuhusu-sura-hii/