Kanuni zifuatazo zitaongoza Vifungu vyote vya fedha za umma katika taifa–
- (a) Kutakuwa na uwazi na uwajibikaji, ikiwa ni pamoja na kuhusika kwa umma katika masuala ya kifedha.
- (b) Mfumo wa fedha za umma utakuza jamii yenye usawa, hasa–
- (i) Mzigo wa utozaji ushuru utasawazishwa;.
- (ii) Mapato yanayopatikana katika kiwango cha kitaifa yatagawanywa sawa kati ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti;.
- (iii) Matumizi yatachangia usawazishaji wa kimaendeleo nchini, ikiwa ni pamoja na mgao maalum kwa makundi ya watu kutoka maeneo yaliyotengwa;
- (c) Mizigo na faida za matumizi ya mapato na ukopaji wa umma itagawanywa sawa kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo;
- (d) fedha za umma lazima zitumiwe kwa busara na uwajibikaji; na
- (e) Usimamizi wa fedha lazima uwajibikiwe vyema na ripoti ya hazina ya serikali iwe wazi.