Ruka hadi Yaliyomo

(1) Hazina ya Mapato ya kila serikali ya Kaunti imeundwa. Hazina hii italipwa pesa zote zilizozalishwa au kupokelewa na, au kwa niaba ya serikali ya kaunti, isipokuwa fedha ambazo kwa sababu maalum zimetengwa na Sheria ya Bunge.

(2) Fedha zinaweza kutolewa kutoka kwa Hazina ya Mapato ya serikali ya Kaunti kwa ajili–

  • (a) Kama malipo dhidi ya Hazina ya Mapato ambayo yamekubaliwa na Sheria ya Bunge au sheria za serikali hiyo ya kaunti; au
  • (b) kama ilivyoidhinishwa na sheria ya matumizi ya fedha katika serikali hiyo ya kaunti.

(3) Fedha hazitatolewa kwa Hazina ya Mapato mpaka Msimamizi wa Bajeti atakapoidhinisha.

(4) Sheria ya Bunge inaweza–

  • (a) kutoa idhini zaidi ya kutoa fedha kutoka kwa Hazina ya Mapato ya Serikali ya Kaunti.
  • (b) kuruhusu serikali za kaunti kuanzisha hazina nyingine za mapato na usimamizi wa hazina kama hizo.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-12/sehemu-2/kifungu-207/hazina-za-mapato-ya-kaunti/