(1) Ni serikali ya kitaifa pekee ambayo imepewa uwezo wa kutoza–
- (a) kodi ya mapato;
- (b) ushuru wa thamani;
- (c) ushuru wa forodha na kodi nyingine katika bidhaa zinazoingizwa na kuuzwa nje ya nchi.; na
- (d) mapato ya ushuru.
(2) Sheria ya Bunge inaweza kuipa mamlaka serikali ya kitaifa kutoza ushuru au kodi nyingine yoyote, isipokuwa ushuru uliotajwa katika ibara ya (3) (a) na (b).
(3) Serikali ya kaunti inaweza kutoza–
- (a) ushuru kwa mali;
- (b) kodi za burudani; na
- (c) na kodi nyingine yoyote ambayo imeruhusiwa na Sheria ya Bunge.
(4) Serikali ya kitaifa na serikali za kaunti zinaweza kutoza ushuru wa huduma.
(5) Utozaji ushuru na mamlaka mengine ya kuzalisha mapato ya serikali ya kaunti hautafanywa kwa njia ambayo inakiuka sera za kiuchumi za kitaifa, shughuli za kiuchumi zinazotekelezwa ndani ya mipaka ya kaunti au uzungushwaji wa bidhaa katika nchi nzima, huduma, mtaji au ajira.