Ruka hadi Yaliyomo

(1) Kutabuniwa Tume ya Ugavi wa Mapato.

(2) Tume hii itajumuisha watu wafuatao watakaoteuliwa na Rais–

  • (a) Mwenyekiti atakayeteuliwa na Rais na kuidhinishwa na Baraza la Kitaifa;
  • (b) Watu wawili walioteuliwa na vyama vya kisiasa vinavyowakilishwa katika Baraza la Kitaifa kutegemea idadi ya wabunge wa chama bungeni;
  • (c) Watu watano walioteuliwa na vyama vya kisiasa vinavyowakilishwa katika seneti kwa kutegemea idadi yao ya uwakilishi katika seneti; na
  • (d) Katibu Mkuu katika wizara inayosimamia fedha.

(3) Watu watakaoteuliwa kwa mujibu wa ibara ya (2) hawatakuwa wabunge.

(4) Ili kuhitimu kuwa kamishna wa Tume hii chini ya ibara ya (2) (a), (b) au (c), mtu lazima awe na tajriba pana katika taaluma ya masuala ya kifedha na uchumi.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-12/sehemu-4/kifungu-215/tume-ya-ugavi-wa-mapato/