Ruka hadi Yaliyomo

(1) Kipindi kisichopungua miezi miwili baada ya kukamilika kwa mwaka wa kifedha, bungeni kutawasilishwa–

  • (a) mswada wa kugawa mapato, ambao utagawa mapato yaliyozalishwa na serikali ya kitaifa kwa serikali za kaunti kwa mujibu wa Katiba hii; na
  • (b) mswada wa kutenga mapato kwa serikali za kaunti, ambao utazigawia serikali za kaunti na mapato yaliyotengwa kwa serikali za kaunti katika misingi ya pendekezo lililoamuliwa chini ya kifungu cha 217.

(2) Kila mswada unaohitajika na ibara ya (2) utaambatanishwa na memoranda itakayoweka wazi–

  • (a) maelezo ya mgao wa mapato kama ilivyopendekezwa na mswada;
  • (b) utathmini wa mswada katika misingi ya kigezo kilichotajwa kwenye Kifungu cha 203 (1); na
  • (c) mukhtasari wa tofauti zozote muhimu kutoka kwa mapendekezo ya Tume, na maelezo kwa kila tofauti iliyopo.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-12/sehemu-4/kifungu-218/miswada-ya-ugavi-wa-mapato/