Ruka hadi Yaliyomo

(1) Iwapo sheria ya matumizi ya fedha haitakuwa imeidhinishwa kufikia mwanzo wa mwaka wa fedha, Baraza la Kitaifa linaweza kuamuru kutolewa kwa pesa kutoka Mfuko wa Jumla wa fedha.

(2) Fedha zitakazotolewa chini ya ibara ya (1)–

  • (a) zitatumiwa kwa minajili ya kuendesha shughuli muhimu za serikali ya kitaifa katika mwaka huo hadi wakati ambapo mswada wa matumizi ya fedha utakapoidhinishwa;
  • (b) kwa jumla zisizidi nusu ya fedha zilizopendekezwa katika makadirio ya matumizi ya mwaka huo yaliyowasilishwa bungeni; na
  • (c) ziwekwe katika vitengo tofauti vya matumizi kwa sababu ya huduma mbalimbali zilizokusudiwa katika mswada wa matumizi ya fedha.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-12/sehemu-5/kifungu-222/matumizi-kabla-kuidhinishwa-bajeti/