Ruka hadi Yaliyomo

(1) Sheria ya Bunge itaidhinisha, kuanzishwa, na kuipa majukumu Hazina ya Kitaifa.

(2) Bunge litapitisha sheria itakayohakikisha usimamizi wa matumizi na uwajibikaji katika serikali zote na kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba zimetekelezwa.

(3) Sheria inayotajwa katika ibara ya (2) inaweza kuamuru waziri anayehusika na fedha kusimamisha uhamishaji wa fedha kwa kitengo fulani cha serikali au shirika lolote la serikali–

  • (a) iwapo tu kuna ukiukaji uliokithiri mipaka au ukiukaji wa kila mara wa hatua zilizowekwa na sheria; na
  • (b) kulingana na masharti ya ibara ya (4) na (7).

(4) Uamuzi wa kusimamia uhamishaji wa fedha kama ilivyoelezwa katika Ibara ya (3) haiwezi kusimamisha uhamishaji wa zaidi ya asilimia hamsini ya fedha zilizotengewa serikali ya kaunti.

(5) Uamuzi wa kusimamisha uhamishaji wa fedha kama ilivyoelezwa katika Kifungu cha (3)–

  • (a) hauwezi kusimamisha uhamishaji kwa siku zaidi ya sitini; na
  • (b) unaweza kutekelezwa mara moja, lakini unaweza kufanya kinyume ila tu, kati ya siku thelathini baada ya tarehe ya maamuzi hayo, Bunge linauidhinisha kwa pendekezo linalopitishwa na viwango vyote mawili vya Bunge.

(6) Bunge linaweza kuweka upya uamuzi wa kusimamisha uhamishaji wa fedha lakini kwa siku zisizozidi sitini kwa wakati mmoja.

(7) Bunge linaweza kuidhinisha au kuweka upya uamuzi wa kusimamisha uhamishaji wa fedha isipokuwa–

  • (a) Msimamizi wa Bajeti amewasilisha ripoti kuhusu suala hili Bungeni; na
  • (b) shirika hilo la umma lipewe nafasi ya kujibu madai dhidi yake, na kujitetea mbele ya kamati husika ya Bunge.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-12/sehemu-6/kifungu-225/udhibiti-wa-fedha/