Ruka hadi Yaliyomo

(1) Sheria ya Bunge itawezesha–

  • (a) kuhifadhi na kukaguliwa kwa rekodi za fedha za serikali na mashirika mengine ya umma, na kuweka hatua za kuhakikisha usimamizi wazi na madhubuti wa fedha; na
  • (b) kuweka Afisa wa Uhasibu katika kila shirika la umma kwenye kiwango cha kitaifa na katika serikali za kaunti.

(2) Afisa wa Uhasibu wa shirika la umma katika kiwango cha kitaifa anawajibikia Baraza la Kitaifa kwa usimamizi fedha katika shirika hilo, na afisa wa uhasibu wa shirika la umma katika kiwango cha kaunti anawajibikia baraza la kaunti kwa usimamizi wa fedha.

(3) Kwa mujibu wa ibara ya (4), hesabu za vitengo vya serikali na nchi zitakaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu.

(4) Hesabu za mkaguzi mkuu wa mahesabu zitakagulia na ripoti kutolewa na mhasibu atakayeteuliwa na Baraza la Kitaifa.

(5) Mhudumu wa Afisi ya Umma, ikiwa ni pamoja na afisi ya kisiasa, akiamuru au kuidhinisha matumizi ya fedha za umma kinyume na sheria au maagizo, mtu huyu atawajibikia hasara yoyote itakayotokana na matumizi hayo na atagharimia hasara hiyo, angali akiwa afisini au la.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-12/sehemu-6/kifungu-226/akaunti-na-ukaguzi-wa-mashirika-ya-umma/