(1) Wakati kitengo cha serikali au shirika lolote la umma linaponunua bidhaa au huduma, ununizi huo utafanywa kwa njia ya haki, usawa, uwazi, yenye ushindani na ya kupunguza gharama.
(2) Sheria ya Bunge itatoa mwongozo wa jinsi sera zinazohusishwa na ununuzi na uuzaji wa mali zitavyotekelezwa na itaamuru kuzingatiwa kwa suala mojawepo au masuala yote yafuatayo–
- (a) vigezo vya kupewa kipaumbele wakati wa kutoa idhini za ununizi;
- (b) kuwalinda na kuwatetea watu, au makundi ya watu ambao awali walinyanyaswa na ushindani usio na haki au uliowatenga;
- (c) kuweka vikwazo dhidi ya wanakandarasi ambao utendakazi wao hautimizi viwango vilivyokubaliwa kitaaluma, kimapatano au kisheria; na
- (d) kuweka vikwazo dhidi ya watu wanaokiuka ulipaji kodi, au ambao wamehusika kwenye ufisadi au wenye makosa makubwa ya ukiukaji wa sheria za uajiri kwa haki.