Ruka hadi Yaliyomo

(1) Kutakuwa na Msimamizi wa Bajeti atakayependekezwa na Rais, kuidhinishwa na Baraza la Kitaifa na kuteuliwa na Rais.

(2) Mtu atakayehitimu kuwa Msimamizi, lazima awe na ujuzi mkubwa wa masuala ya fedha za umma au tajriba isiyopungua ya miaka kumi katika ukaguzi na usimamizi wa fedha za umma.

(3) Msimamizi wa Bajeti, chini ya Kifungu cha 251, atahudumu kwa kipindi cha miaka nane na hataweza kuteuliwa tena.

(4) Msimamizi wa Bajeti atasimamia utekelezaji wa bajeti ya kitaifa na bajeti za serikali za kaunti kwa kuagiza kutolewa kwa fedha kutoka kwa hazina za umma chini ya Kifungu cha 204, 206 na 207.

(5) Msimamizi huyu hataidhinisha kutolewa kwa fedha kutoka kwa hazina za umma mpaka aridhike kuwa utowaji huo umekubalika kisheria.

(6) Kila baada ya miezi minne, Msimamizi huyu atawasilisha kwa mabaraza yote ya Bunge ripoti ya utekelezaji wa bajeti ya kitaifa na bajeti za serikaliza kaunti.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-12/sehemu-7/kifungu-228/msimamizi-wa-bajeti/