(1) Maadili na Kanuni za Umma huhusisha–
- (a) viwango vya juu vya maadili ya kitaaluma;
- (b) matumizi bora ya rasilmali;
- (c) utoaji wa haraka wa huduma za umma usio na upendeleo na unaozingatia usawa na haki;
- (d) ushirikishwaji wa watu katika utaratibu wa kuunda Sera;
- (e) uwajibikaji katika shughuli za kiusimamizi;
- (f) uwazi na utoaji wa habari sahihi kwa umma bila kuchelewa;
- (g) kwa kuzingatia ibara za (h) na (i), ustahili na ujuzi wa mtu ndio msingi wa kuteuliwa au kupandishwa cheo;
- (h) uwakilishi wa jamii mbalimbali za Kenya; na
- (i) kutoa nafasi sawa na za kutosha za kazi, katika kuteua, kutoa mafunzo na kupandishwa vyeo katika ngazi zote zahuduma za umma, kwa–
- (i) wanaume na wanawake;
- (ii) watu wa jamii zote; na
- (iii) watu wenye ulemavu.
(2) Maadili na Kanuni za Huduma za umma huhusisha huduma za umma kwa–
- (a) idara zote za serikali katika viwango vyote viwili vya serikali; na
- (b) mashirika yote ya serikali.
(3) Bunge litaunda sheria kukipa nguvu Kifungu hiki.