Ruka hadi Yaliyomo

(1) Chini ya utaratibu uliosawazishwa na kanuni zilizoidhinishwa na Sheria ya Bunge, serikali ya kaunti ina wajibu wa–

  • (a) kuunda na kuvunja afisi katika huduma za umma;
  • (b) kuteua watu kuhudumu au kushikilia kwa muda afisi katika huduma za umma, kuidhinisha uteuzi ; na
  • (c) kudumisha nidhamu pamoja na kuwaachisha kazi watu wanaohudumu katika ofisi hizo au wanaozishikilia kwa muda.

(2) Ibara ya (1) haitazingatiwa katika afisi yoyote au wadhifa wowote unaohusu Tume ya Kuwaajiri Walimu.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-13/sehemu-2/kifungu-235/kuajiri-wafanyikazi-wa-kaunti/