(1) Tume ya Kuwaajiri Walimu imeundwa.
(2) Majukumu ya Tume ni–
- (a) kusajili walimu waliohitimu;
- (b) kuteua na kuajiri walimu waliosajiliwa;
- (c) kuwapa kazi walimu walioajiriwa na Tume hii kuhudumu katika shule yoyote ya umma au taasisi;
- (d) kuwapandisha vyeo na kuwahamisha walimu;
- (e) kushughulikia masuala ya kinidhamu ya walimu; na
- (f) kuwafuta kazi walimu.
(3) Tume–
- (a) itachunguza viwango vya elimu na mafunzo kwa watu wanaojiunga na taaluma ya ualimu;
- (b) itachunguza kuhitajika kwa walimu na upatikanaji wao; na
- (c) itashauri serikali ya kitaifa kuhusu masuala yanayohusiana na taaluma ya ualimu.