(1) Huduma za Polisi za Kitaifa–
- (a) zitajitahidi kufikia viwango vya juu vya kitaaluma na kinidhamu miongoni mwa wafanyakazi wake;
- (b) zitazuia ufisadi, kukuza na kutekeleza uwazi na uwajibikaji;
- (c) zitazingatia viwango vya kikatiba vya haki za binadamu na uhuru wa kimsingi;
- (d) zitawapa wafanyikazi wake mafunzo hadi kufikia viwango vya juu zaidi vya kitaaluma na kimaadili kwa wafanyikazi wake, na kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa kimsingi; na
- (e) zitajenga na kukuza mahusiano na jamii pana.