(1) Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa imeundwa.
(2) Tume inahusisha–
- (a) watu wafuatao, kila mmoja wao akiwa ameteuliwa na Rais-
- (i) mtu anayestahili kuteuliwa kama Jaji wa Mahakama ya Juu;
- (i) maafisa wawili wa polisi wa ngazi za juu waliostaafu; na
- (ii) watu watatu wenye maadili mema ambao wamewahi kuhudumu serikalini kwa umahiri mkubwa.
- (b) Inspekta-Mkuu wa Huduma za Polisi za Kitaifa.
- (c) Manaibu wote wawili wa Inspekta-Mkuu wa Huduma za Polisi za Kitaifa.
(3) Tume–
- (a) itaajiri na kuteua watu kuhudumu au kushikilia kwa muda afisi za huduma hiyo, kuidhinisha uteuzi na kuamua watakaopandishwa vyeo na kuhamishwa katika huduma za polisi za kitaifa.
- (b) itazingatia utaratibu wa sheria, kutekeleza majukumu ya kinidhamu na kuwaondoa watu wanaohudumu au kushikilia kwa muda afisi za huduma hii; na
- (c) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa sheria ya nchi..
(4) Uajiri katika Huduma za Polisi za Kitaifa utabainisha tofauti za kimaeneo na za jamii mbalimbali za watu wa Kenya.